Deep Sea Fish Oil Capsule
Viungo:
Deep Sea Fish Oil Extract, EPA: 180mg/capsule; DHA: 120mg/capsule
Kazi na Faida zake:
- Kupunguza kiwango cha lipids (mafuta kama cholesterol na triglycerides) vinavyozunguka katika mfumo wa damu,
- Kupunguza uvimbeuchungu (inflammation) ulioko sehemu mbalimbali za mwili
- Kupunguza kuongezeka kwa vipande vya protoplasm (platelet) vilivyoko ndani ya damu; Kuzuia damu isigande kupita kiasi
- Kuzuia arteri zisiongezeke unene; kupanua na kulegeza arteri.
Inafaa Kutumika Kwa:
- Watu wenye matatizo ya mishipa ya moyo na mishipa ya ubongo
- Watu wenye kisukari, Type 2 diabetes
- Watu wenye matatizo ya mifupa na maungio ya mifupa kama osteoporosis na arthritis.
- Watu wenye umri mkubwa wanaoshindwa kupata chakula chenye mafuta ya omega-3 ya kutosha
Maelezo Muhimu:
Utafiti umegundua kuwa baadhi ya mafuta (fats) ni mazuri kwa afya ya binadamu na kuwa ni muhimu katika ufanyaji kazi wa mwili. Mafuta haya ni kama Omega-3, Omega-6 na Omega-9. Mafuta haya huitwa unsaturated fats au polyunsaturated fats. Miili ya binadamu haina vimeng'enya (enzymes) vya kutengeneza mafuta ya omega-3 na omega-6, kwa hiyo tunahitaji kuyapata kutokana na chakula tunachokula. Upungufu wa mafuta hayo mwilini husababisha magonjwa. Hii ndiyo sababu mafuta haya huitwa mafuta muhimu ya mwili (essential fat acids).
Mafuta Ya Omega-3 (Omega-3 Fatty Acids)
Aina tatu za mafuta ya omega-3 ambazo ni muhimu sana kilishe ni alpha-linolenic acid (ALA), eicosapentaenoic acid (EPA) na docosa-hexaenoic acid (DHA), aina za mafuta ambazo zinaweza pia kupatikana moja kwa moja kutokana na chakula cha aina fulani, hasa kutokana na samaki wa maji baridi ikiwa ni pamoja na salmon, tuna, halibut na herring.
EPA ina mchango mkubwa katika kuzuia magonjwa ya mishipa ya moyo, wakati DHA ni muhimu katika kuhakikisha ufanyaji kazi mzuri na ukuaji wa ubongo na neva. Mafuta ya Omega-6, ambayo mara nyingine huitwa linoleic acid, yana faida katika ukuaji wa mfumo wa neva na katika ukarabati wa ngozi. Omega-9, ambayo huitwa oleic acid, husaidia kutunza mishipa ya damu na kuimarisha kinga za mwili.
Kwa Utando Wa Seli Wenye Afya (Healthy Cell Membranes)
Kusudi seli iweze kufanya kazi zake kikamilifu, utando wa nje wa seli (cell membrane) unatakiwa uwe na ukamilifu na ugiligili (hali ya ulaini au kama kimiminiko). Seli zinazokosa utando wenye afya hupoteza uwezo wa kutunza maji na virutubishi muhimu. Seli hizo hupoteza uwezo wa kupitisha taarifa kutoka seli moja hadi nyingine. Utafiti unaonyesha kuwa ukosefu wa mawasiliano kutoka seli moja hadi nyingine ni moja ya vyanzo vinavyopelekea kujenga uvimbe wa saratani.
Kwa sababu utando wa seli hujengwa na mafuta, ukalifu na ugiligili wa utando huo hutegemea sana aina ya mafuta tunayokula. Kumbuka kuwa mafuta mengine (saturated fats) huwa ni magumu (solids) kwenye halijoto ya kawaida, wakati mafuta ya omega-3 huwa ni kimiminiko kwenye halijoto ya kawaida. Watafiti wanaamini kuwa chakula chenye kiwango kikubwa cha saturated fats au hydrogenated fats hutengeneza utando wa seli ulio mgumu na hukosa ugiligili. Kwa upande mwingine, chakula chenye uwingi wa omega-3 hutengeneza utando wa seli wenye ugiligili wa hali ya juu.
Kuzuia Uvimbeuchungu (Anti-inflammatory)
Kugundulika kwa zao la lipid lijulikanalo kama Resolvins, ambalo linatengenezwa na miili yetu kutokana na EPA, kunaeleza kwa nini mafuta ya omega-3 yanazuia uvimbe kwenye maungio ya mifupa na kuboresha mzunguko wa damu.
Resolvins zinatengenezwa kutoka EPA na vimeng'enya vya seli (cellular enzymes) na hufanya kazi kwa kuzuia utengenezaji na kudhibiti usambaaji wa seli na kemikali za uvimbe kuelekea kwenye sehemu iliyoumia. Tofauti na dawa za kuzuia uvimbe kama aspirin, ibuprofen na vinginevyo, resolvins za kwenye miili yetu hazina madhara kwenye viungo vya tumbo na mishipa ya moyo.
Faida Kwenye Michipa Ya Moyo Na Mishipa Ya Ubongo
EPA na DHA hupunguza hali zinazoweza kusababisha magonjwa ya moyo, ikiwa ni pamoja na kuwa na cholesterol kwa wingi na kuwa na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure).
Deep Sea Fish Oil imeonekana kuwa na uwezo wa kupunguza viwango vya triglycerides, na hivyo, kupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la damu, kifo, kiharusi na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida kwa watu ambao walishapatwa na shinikizo la damu. Deep Sea Fish Oil inasaidia kuzuia na kutibu tatizo la kupungua kwa kipenyo cha mishipa ya damu (atherosclerosis) kwa kupunguza ujengwaji wa tabaka (plaque) la mafuta juu ya kuta za ndani za mishipa na kuzuia kuganda kwa damu, ambavyo vinasababisha kuziba kwa mishipa ya arteri.
Faida Kwa Wenye Kisukari
Watu wenye kisukari wana kiwango kikubwa cha triglycerides (mafuta ndani ya damu) na kiwango kidogo cha HDL (cholesterol nzuri kwa afya). Aina nyingine ya mafuta ya omega-3, ALA (kwa mfano,kutoka mbegu za mimea kama flaxseed, haziwezi kuwa na ubora kama Deep Sea Fish Oil. Watu wengine wenye kisukari hawawezi kubadilisha ALA kwenda EPA na DHA. Kupata Deep Sea fish Oil ni muhimu kwa wale wenye kisukari cha aina ya Type 2 diabetes.
.
<<<<< MWANZO